Condition: New,UPC: 9781987771336,Publication Date: Sun, April 1, 2018,Type: Paperback ,
description
3Chozi la Sundi ni hadithi inayomwelezea binti mdogo mwenye ulemavu wa ngozi anayeishi kijijini kwenye jamii ya kabila la wasukuma wanaopatikana nchini Tanzania. Katika hadithi hii mwandishi ameonesha namna mila na desturi za kiafrika zinavyowanyanyasa watu wenye mahitaji maalumu kama walemavu wa ngozi na vikongwe. Walemavu wa ngozi wananyanyaswa, wanatengwa na jamii pia wanawindwa kuuawa kwa imani potofu. Vikongwe nao wanawindwa kuuawa kwa imani kuwa ni washirikina wanaokwamisha maendeleo. Natumaini kuwa itatoa mafundisho mengi kwa jamii kuepukana na mauaji ya vikongwe na albino na kuonesha umuhimu wa kuthamini haki ya kila mtu kuishi kama ilivyo katika mikataba ya kimataifa na katiba za nchi mbalimbali.